Quantcast
Channel: SPOTI Starehe™
Viewing all 699 articles
Browse latest View live

Noma raphael daudi aweka rekodi kwa goli lake kimataifa

$
0
0
Na George Mganga 
Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Raphael Daud, jana aliweka rekodi yake katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Daud aliifungia Yanga bao la kwanza katika sekunde ya 27 tu ya mchezo, likiwa ni bao la mapema zaidi kwenye michuano hiyo msimu huu.
Bao hilo linatengeneza rekodi kwa Daudi na Yanga kwa ujumla kutoa mchezaji aliyeweza kucheka na nyavu ndani ya nusu dakika dhidi ya Wolaitta Dicha SC kutoka Ethiopia.
Yanga iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Bao jingine la Yanga lilifungwa na Mshambuliaji Emmanuel Martin kwa njia ya kichwa katika dakika ya 54 ya kipindi cha pili.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kujitengenezea mazingira mazuri ya kuingia hatua ya makundi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki moja baadaye huko Ethiopia

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Matokeo ligi kuu bara leo

$
0
0

Na George Mganga 

Kivumbi cha Ligi Kuu Bara kimeendelea tena jioni ya leo kwa viwanja vinne kuwaka moto.

Katika mchezo uliopigwa huko Shinyanga, wenyeji Stand United wametoa dozi ya mabao 3-1 dhidi ya Njombe Mji FC kutoka Njombe.

Mbao ya Stand United yamefungwa na Suleiman Ndikumana katika dakika ya kwanza ya mchezo huku mengine yakitiwa kimiani na Sixtus Sabilo kwenye dakika za 84 na 90. Bao pekee la Njombe Mji limefungwa na Notkelly Masasi katika dakika ya 75.

Wakati huohuo Kagera Sugar imelazimisha sare ya mabao 1-1 dhidi ya Ndanda FC katika dimba la Nangwanda Sijaona huko Mtwara, Ndanda wamejipatia bao lao kupitia Mrisho Ngassa (33') na Kagera wakijipatia goli kupitia Abdallah Mguhi ( 27').

Matokeo ya mechi zingine yalikuwa ni suluhu ya 0-0 kwa Mbeya City iliyoikaribisha Azam FC huko Mbeya, Sokoine Stadium. Ruvu Shooting nayo ikalazimishwa suluhu ya kutofungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Simba fiti kuwakabili mtibwa kesho

$
0
0
Na George Mganga 
Kikosi cha Simba kinafanya mazoezi ya mwisho mjini Morogoro leo, tayari kwa mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa mjini Morogoro kesho Jumatatu.
Simba na Mtibwa zitakuwa zinaingia Jamhuri zikiwa na kumbukumbu ya kupata matokeo kwenye mechi zilizopita, ambapo Simba iliiadhibu Njombe Mji kwa mabao 2-0 huku Mtibwa ikiilaza vikali Singida United 3-0, michezo yote ikipigwa ugenini.
Simba itakuwa kibaruani bila wachezaji wake muhimu watatu ambao wanatumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano.
Beki Juuko Murushid, Erasto Nyoni na Kiungo James Kotei hawataitumikia timu yao kesho sababu ya kuwa na idadi ya hiyo ya kadi za njano, hivyo watalazimika kuisubiri Tanzania Prisons kwenye unaofuata baada ya Mtibwa Sugar.
Licha ya kukosekana wachezaji hao, Kiungo Jonas Mkude anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kufuatia kupona majeraha yake ya kifundo cha mguu aliyoyapata wiki moja iliyopita wakati timu ikijiandaa na mchezo dhidi ya Njombe Mji.
Mkude aliumia kifundo hicho baada ya kukwaana miguu na kiungo mwenzake, Mzamiru Yassin kwenye Uwanja wa Boko Vetarani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Habari kubwa za Magazeti ya TZ leo Jumatatu April 9 2018 Udaku, Michezo na Hardnews

$
0
0
Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania Jumatatu April 9 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa























Kesi ya Zuma kusikilizwa tena mwezi june.

$
0
0

Rais wa zamani wa Afrika Kusini anayeshtakiwa kwa makosa ya rushwa inayohusishwa na mpango wa silaha wa mwaka 1990.

Mara baada ya Bwana Zuma kuwasili katika mahakama kuu huko Durban hapo jana kwa kipindi cha dakika 15,kesi yake ilihairishwa mpaka tarehe 8 mwezi juni.

Bwana Zuma ambaye anakabiliana na mashtaka 16 ya ufisadi,rushwa ,udanganyifu aliofanya ili kujipatia fedha na utakatishaji wa fedha
Bwana Zuma alilazimika kuachia madaraka yake mwezi februari licha ya kukataa kuhusika na kosa lolote.

Wafuasi wake walisambaa mjini wakiandamana kwa ajili yake huku wapinzani wake walilalamika kwamba mahakama inachukua muda mrefu kutoa hukumu.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa,Bwana Zuma aliwahutubia mkusanyiko wa watu waliomsindikiza mahakamani kutoka nyumbani kwake.

"Sijawahi kuona mtu anashtakiwa kwa uhalifu, alafu mashtaka yake yanafutwa lakini baada ya miaka kadhaa ,mashtaka hayohayo yanarejeshwa" ,Zuma alisema.

"Hizi ni njama za kisiasa"

Baada ya hapo Bwana Zuma aliongoza nyimbo na kucheza pamoja na wafuasi wake.

Mpango wa silaha ulikuwa ni upi?

Mpango wa silaha ulifanyika mwaka 1999 mwaka ambao bwana Zuma alihama kutoka mkuu wa jimbo kuwa makamu wa rais.

Anashtakiwa kwa kukubali kuchukua malipo yasiyokuwa halali 783
Mshauri wake wa mambo ya fedha ,Schabir Shaikh alikutwa na hatia kwa kujaribu kuomba rushwa kwa niaba ya bwana Zuma kutoka katika kampuni ya silaha za Ufaransa na kosa hilo lilipelekea akafungwa jela mwaka 2005.
Kesi dhidi ya bwana Zuma ilifutwa muda mfupi kabla hajawania nafasi ya uraisi mwaka 2009.

Posted by Lebabtv
Source: Bbc Swahili

Harry Kane anaamini atamshinda Mohamed Salah kwa ufungaji wa mabao.

$
0
0





Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane amesema anaamini atamshinda nyota wa Liverpool Mohamed Salah na kutwaa tuzo ya mfungaji mabao bora Ligi ya Premia msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa England amefunga mabao 24 msimu huu.
Hata hivyo, ameachwa nyuma na Salah ambaye ni raia wa Misri kwa mabao matano.

Kane, 24, anapigania kuwa mchezaji wa kwanza tangu Thierry Henry kuongoza kwa ufungaji wa mabao Ligi Kuu ya England kwa misimu mitatu mtawalia.

"Naamini ninaweza kufanya hivyo. Bado kuna mechi zilizosalia kuchezwa," Kane amesema.

"Lazima niendelee kuangazia uchezaji wangu. Siwezi kudhibiti anachofanya yeye

"Bila shaka kama mshambuliaji, itakuwa vyema sana kuishinda buti ya dhahabu tena na nitaendelea kutia bidhii kuanzia sasa hdi mwisho wa msimu."


Kane ambaye amekuwa akiuguza jeraha la kifundo cha mfuu amerejea kucheza baada ya kupona.

Mshindani wake Salaha, 25, hata hivyo hakucheza debi ya Merseyside Jumamosi kutokana na jeraha la mtoki alilopata akichea Liverpool mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano ambapo waliwalaza Manchester City mechi ya mkondo wa kwanza robo ainali.

Kane ana nafuu kidogo ukizingatia kwamba Spurs wamesalia na mechi sita za kucheza Ligi Kuu lakini Liverpool wana mechi tano pekee.

Na huenda bado akafaidika zaidi katika kupunguza mwanya kati yake na Salah iwapo atahesabiwa bao la ushindi dhidi ya Stoke Jumamosi, ingawa kituo cha wasimamizi wa mechi cha Ligi ya Premia siku hiyo kiliamua kwamba Christian Eriksen ndiye aliyefunga bao hilo.





Spurs walilaza Stoke 2-1. Mabao yote mawili yalihesabiwa kuwa ya Eriksen.

Kane anasisitiza kwamba mpira frikiki iliyopigwa na Eriksen ulimgusa begani kabla ya kumbwaga kipa wa Stoke Jack Butland na kuingia wavuni.

Spurs wamepanga kukata rufaa uamuzi huo wa kumpa kiungo huo wa kati kutoka Denmark bao hilo na badala yake wanataka lihesabiwe kuwa la Kane "Naapa kwa uhai wa binti wangu kwamba niliuguza mpira huo, lakini hakuna jambo jingine ninaloweza kulifanya," Kane amesema.

"Wakiamua kubadilisha, watabadilisha. Wakiamua kuamini msimamo wangu, watakuwa wameusikia msimamo wangu.
"Mambo ni vile yalivyo - muhimu zaidi ni kwamba tulishinda mechi".

WAFUNGAJI 10 MABAO EPL MPAKA SASA HIVI..
Mohamed Salah, Liverpool 29
Harry Kane, Tottenham 24
Sergio Agüero, Man City 21
Raheem Sterling, Man City 16
Jamie Vardy, Leicester 16
Romelu Lukaku, Man Utd 15
Roberto Firmino, Liverpool 14
Son Heung-min, Tottenham 12
Álvaro Morata, Chelsea 11
Eden Hazard, Chelsea 11

Posted by Lebabtv
Source: The Guardian

Tetesi za soka Ulaya. Mpango wa kumchukua Fellaini, Fred atafutwa na Man Utd na City, Cresswell, Ribery, Robben, Mourinho

$
0
0
Liverpool wameandaa mkataba wa miaka mitatu kwa ajili ya mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Mbelgiji Marouane Fellaini, huku Paris St-Germain na Monaco pia wakionyesha kumtaka kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye mkataba wake katika Old Trafford unamalizika mwisho wa msimu. (L'Equipe -kwa Kifaransa)


Manchester United wana matumani ya kuwaadhibu zaidi mahasimu wao Manchester City kwa kusaini mkataba na Shakhtar Donetsk na mchezaji wa safu ya kati wa Brazil Fred, 25, mwisho wa msimu. (Mirror)
Mkuu wa zamani wa waamuzi England Keith Hackett haelewi ni kwa nini Martin Atkinson hakumfukuza wuanjani beki wa Manchester United Ashley Young wakati wa mechi yao dhidi ya Manchester City. Amesema vitendo vya Atkinson ni thibitisho tosha ya kuonesha ni kwa nini waamuzi wa England waliachwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu. (Telegraph)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema klabu hiyo haistahili kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iwapo haiwezi kuzishinda timu kama vile West Ham. Hii ni baada ya klabu hiyo kutoka sare ya 1-1 na West Ham. (Times)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema pendekezo la Manchester City kwamba klabu hiyo inaweza kutumia uwanja wake wa mazoezi kwa maandalizi ya mechi ya marudiano ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne lilitolewa kwa kuchelewa

Manchester United pia walikataa ombi kutoka kwa Liverpool wa kutumia uwanja wao wa timu ya wachezaji chipukizi. (Telegraph)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema huenda ndiye anayefaa kulaumiwa kwa klabu hiyo kulazwa na Liverpool na Manchester United. Hata hivyo amesema kutomakinika mbele ya lango kuna maana kwamba timu hiyo bado haijatosha kushindana katika ligi kuu bara Ulaya. (Times)
Everton inataka kutumia Euro milioni 25 majira ya joto yajayo kumnunua mchezaji wa West Ham Aaron Cresswell, mwenye umri wa miaka 28 ambaye pia ni beki wa kushoto katika timu ya England . (Sun)
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anasema Pep Guardiola alidai Manchester City walipewa nafasi ya kumsajili Paul Pogba mwezi Januari kulipiza kisasi dhidi ya ajenti wake Mfaransa Mino Raiola. (Mirror)
Mourinho alionekana kugongwa na sarafu ya pauni iliyotupwa kutoka kwenye umati wa mashabiki wakati wa mechi ambayo Manchester United walishinda dhidi ya Manchester City Jumamosi, lakini Mreno huyo hakuripoti tukio hilo. (Star)

Bayern Munich watatoa fursa ya kusaini mkataba mpya kwa Mfaransa Franck Ribery, mwenye umri wa miaka 35, na Mholanzi Arjen Robben, mwenye umri wa miaka 34, ambao mikataba yao ya sasa inamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Bild - kwa Kijerumani)
Mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham Christian Eriksen anasema kumekuwa na malumbano ndani ya chumba cha kuvalia jezi za mpira juu ya ikiwa yeye ama Harry Kane ndiye anayefaa kutambuliwa kama mfungaji wa goli la pili la Spurs dhidi ya Stoke katika mechi ya Jumamosi ambayo walishinda 2-1. (Independent)
Mshambuliaji wa timu ya Sheffield Wednesday- George Hirst mwenye umri wa miaka 19 - mwana wa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo David - anatarajiwa kujiunga na Manchester United, huku klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship ikitarajia kufaidi kutokana na hatua hiyo. (Mirror)
Viongozi wa Ligi ya Uholanzi PSV Eindhoven wanasema Everton wameonyesha nia ya kumtaka mkurugenzi wao wa soka Marcel Brands. (Sky Sports)

Mchezaji wa safu ya kati wa QPR Stephane Mbia, mwenye umri wa miaka 31, yuko tayari kuhamia klabu ya Atlanta inayocheza Ligi Kuu ya Marekani Kaskazini (MLS) kwa uhamisho wa bila malipo. (ESPN)
Kipa wa West Brom Ben Foster, 35, anataka kusalia katika klabu hiyo hata ikishushwa daraja kutoka Ligi ya Premia.
Kiungo wa kati wa Liverpool Mjerumani Emre Can, 24, ambaye mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huenda akaamua mustakabali wake katika kipindi cha wiki mbili zijazo, kwa mujibu wa mkuu wa Juventus Beppe Marotta. (Mediaset Premium, kupitia Express)
Posted By LebabTv
Source: Bbc Swahili

Download Upya Application Yetu Ya Spoti

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya Spoti Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Maboresho Mapya Yamefanyika ili kukufanya upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyokua

App ya zamani ilikuwa na tatizo kubwa la kuchelewa kufunguka, kuchelewesha habari na muonekano wake haukuwa wa kiwango kinachostahili.

Chakufanya, Ingia PlayStore, Download Upya Application yetu  MPYA. Ukishaipakua hii Mpya, ya zamani ifute tu.

NB: App mpya ina Icon ya Mpira wa Moto

Tumekurahisishia; 


Mtibwa Sugar kuivurugia Simba Leo Bila Okwi

$
0
0

Harakati wa kusaka ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2017/18, zinaendelea leo kwa mchezo mmoja utakaoshuhudia Wekundu Wa Msimbazi Simba wakipapatuana na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.
Simba ambao ndiyo vinara wa ligi hiyo kwa sasa, watalazimika kusaka ushindi ili kujisafishia njia ya kutwaa ubingwa wa Tanzania bara, ambao pia unawaniwa na mahasimu wao katika soka la bongo Young Africans.
Hata hivyo Simba wataingia uwanjani hii leo huku wakiwakosa wachezaji wao watatu kutokana na kuwa na kadi tatu za njano, ambao ni Erasto Nyoni, Juuko Murshid na James Kotei.
Kabla ya kuwasili mjini Morogoro mwishoni mwa juma lililopita, Simba walikuwa wameweka kambi mkoni Iringa, baada ya ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Njombe Mji.
Kwa wenyeji wa mchezo wa hii leo Mtibwa Sugar ambao wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 30, wamepania kuvuruga rekodi ya Simba ya kutopoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi, kwa kuhakikisha kunaifunga kwa mara ya kwanza na kuondoka na alama tatu muhimu.
Kinachoongeza utamu katika mpambano huo ni kiwango bora cha Mtibwa Sugar kwa siku za karibuni wakiwa imetoka kuwafunga vigogo wawili mfululizo ikianza na Azam FC katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports na kisha kuifunga Singida United mabao mabao matatu kwa sifuri katika mchezo wa ligi.
Chanzo: Dar 24

Jacqueline Wolper apewa Onyo Kali na mpenzi wa Harmonize

$
0
0
Mpenzi wa msanii Harmonize, Sarah amemuonya ex-girlfriend wa muimbaiji huyo Jacqueline Wolper kwa kile alichodai muigizaji huyo anamsumbua sana mpenzi wake katika mitandao.
Aliweka wazi hilo ni Wolper ambaye ameweka wazi jumbe alizotumiwa na Sarah kupitia mtandao wa WhatsApp na kueleza kuwa hawezi kumjibu kwa sasa zaidi ya kumuhurumia.

Harmonize na Wolper walikuwa wapenzi kipindi cha nyuma na couple yao ilikuwa na nguvu sana yenye kukodolewa macho na vijana wengi. Walionekana kushibana katika mapenzi yao kiasi kwamba Harmonize aliweza hata kumshirikisha Wolper katika video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la Niambie.
Baada ya kuachana Harmonize aliweka wazi kuwa katika mahusiano na Sarah binti kutoka nchini Italy na Wolper naye akawa na mahusiano na kijana maarufu mtandaoni, Brown, hata hivyo mahusiano yao pia hayakuchukua muda ukawa umevunjika.

Monalisa Akabidhiwa Bendera Kupeperusha Nchi Ghana

$
0
0
Mwanadada Monalisa ambae ni msanii mkongwe sana katika tasnia ya filamu amekabidhiwa bendera ya taifa pamoja na ticket ya ndege na Mh  waziri wa michezo Harrison Mwakyembe kwa ajili ya safari yake ya kwenda Ghana ambapo ataenda kuepeperusha bendera ya Taifa katika maswala ya tasnia ya filamu kutokana na kuchaguliwa kwake katika kuwania tuzo za African Prestigious Award nchini humo   zitakazofanyika April 14,2018 .

Monalisa ambae alisindikizwa na mama yake  katika makabidhiano hayo katika ofisi za Baraza  walihudhuria pia watu mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Habari sanaa na Michezo Mh .Juliana Shonza pamoja na katibu mtendaji wa baraza la sanaa tanzania.

Monalisa anakwenda kuiwakilisha Tanzania baada ya kuchaguliwa katika kategoria hiyo na kuomba watanzania na afrika kwa ujumla kumpiagia kura kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja sasa.Kila la kheri kwake. 
BY richard@spoti.co.tz

Dj Rasta Bob Wa Uganda Adai Zari Alikuwa Mpenzi Wake Kabla Hajamuacha na Kukimbilia kwa Akina Diamond na Wengine

$
0
0
Dj na mtangazaji maarufu nchini Uganda Robert Ogwel maarufu kama Dj Rasta Bob Mc amefunguka na kudai Ex wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari alikuwa mpenzi wake kabla hajamuacha na kwenda kwa Ivan.

Dj Rasta Bob alimwaga ubuyu huo Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na kituo cha Spark Tv nchini Uganda ambapo alidai yeye ndio alikuwa mwanaume wa kwanza kuwa na Zari.

Dj huyo amefunguka na kudai kuwa yeye ndio alimtoa Zari kwao Jinja na kumleta jijini Kampala nchini Uganda kutokana na kuvutiwa na urembo wake lakini pia amedai kuwa yeye ndio alimfunza mambo mengi Zari kuhusu ustaa kwani kipindi hiko alikuwa maarufu sana.

Lakini pia amedai muda mfupi baada ya kuwa wa mjini na kupendeza ndipo Zari alivyomtosa na kuanza kutoka kimapenzi na mwanaume tajiri ambaye ni Ivan na kumwambia anaweza kuishi mwenyewe mjini na kumuacha solemba.

Dj Rasta ambaye ni mkongwe nchini Uganda katika sekta ya burudani amekiri pamoja kuwa Zari amefanikiwa kimaisha na kutoka na wanaume matajiri lakini watambue kuwa yeye ndio alimtoa kijijini na kumfundisha kila kitu kuhusu kuishi mjini.
 
by richard@spoti.co.tz

Miss Tanzania Yazaliwa Upya,......Mwakyembe Asimulia Alivyokuwa Anakerwa na Uhuni wa Lundenga

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameweka wazi kwamba alikuwa tayari kuchukua mashindano ya Miss Tanzania kutoka kwa muandaaji Hashim Lundenga kwa madai kuwa kulikuwa na uhuni ulioanza kuigubika tasnia hiyo.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Miss Tanzania Mpya chini ya Mkurugenzi wa The Look Company, Miss Tanzania 1998 Bi. Basila Mwanukuzi, Dk Mwakyembe amesema kuwa uhuni wa waandaji ulishamkwaza hivyo kwa kuwa mabadiliko yameangukia mikononi mwa Basila basi anaamini 'upele umepata mkunaji'.

Akizungumzia chanzo cha kutaka kuyaweka mashindano hayo kuwa chini yake kutoka kwenye kampuni ya Lino Agency, Waziri Mwakyembe amesema kwamba alikasirishwa na uhuni aliofanyiwa Miss Tanzania 2016 kwa kupewa zawadi ya gari hewa huku akiongeza kuwa mabinti wanajitoa kwa juhudi licha ya kuwepo kwa mfumo dume kwenye jamii.

"Watotot wa watu wanajitolea, mfumo wetu bado ni dume wanapata tabu sana kuishawishi jamii kuwa haya ni mashindano ya kawaida anapita kwenye chujio anashinda alafu unampa zawadi hewa. Basila mwenyewe aliwahi kupewa zawadi hewa kaeni naye vizuri atawaeleza. hivyo niseme mabadiliko haya yamenifanya nione kwamba upele umepata mkunaji" Mwakyembe.

Hata hivyo Waziri huyo mwenye dhamana ya sanaa amemtaka muandaaji huyo mpya (Basila Mwanukuzi) kuhakikisha anaondoa ubabaishaji wote uliokuwepo na kumuahidi kuwa serikali ipo nyuma yake.
 
by richard@spoti.co.tz

Simba yaendeleza dozi leo ilikuwa mtibwa

$
0
0


Na George Mganga 

Simba SC imeendelea kujikusanyia alama katika Ligi Kuu Bara baada ya kuilaza Mtibwa Sugar FC kwa bao 1-0 jioni hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mchezo huo uliokuwa unaambatana na mvua iliyokuwa ikinyesha Uwanjani, ulishuhudiwa nyavu zikitikiswa mnamo dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza na Emmanuel Okwi.

Okwi alifunga bao hilo akimalizia kazi mpira wa kichwa kutoka kwa John Bocco na kufanya mchezo huo udumu kwa dakika zote 90 huku matokeo yakisalia kuwa 1-0.

Matokeo hayo yanaifanya Simba izidi kujikita kileleni kwa kufikisha alama 52 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga wenye 46 mpaka sasa.

Mechi inayofuatia kwa Simba itakuwa dhidi ya Wajelajela Tanzania Prisons, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Uongozi azam waichana mbeya city

$
0
0


Baada ya mchezo wa ligi kati ya Mbeya City na Azam FC kwenda suluhu ya bila kufungana katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, uongozi wa Azam waitupiwa lawama Mbeya City.

Kupitia Afisa Habari wa Azam, Jaffer Idd Maganga, alisema kuwa wachezaji wa Mbeya hawakuwa wanacheza mpira kupata matokeo bali walipambania pointi moja.

Maganga alieleza kuwa wapinzani wao walikuwa wanatumia muda mwingi kupoteza muda huku akieleza kuwa walikuwa wameridhika ilihali wao walikuwa wanapambana kujipatia alama 3 muhimu.

Azam iliambulia alama moja kwenye mchezo na kuzidi kusalia katika nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi kuu bara ikiwa na pointi 45 huku ikicheza jumla ya michezo 23 mpaka sasa.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email:agape@spoti.co.tz

GUARDIOLA AENDESHA MJADALA MZITO KUELEKEA MECHI NA LIVERPOOL KESHO

$
0
0


Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akijadiliana na wasaidizi wake wakati wa mazoezi ya leo jioni kujiandaa na mchezo wa marudiano Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool Uwanja wa Etihad wakihitaji ushindi wa 4-0 kusonga mbele kufuatia kufungwa 3-0 kwenye mechi ya kwanza Uwanja wa Anfield wiki iliyopita

Raisi wa Sporting Cp awafungia wachezaji 19 wa kikosi cha kwanza.

$
0
0

Boss ni boss tu, hicho ndicho unachoweza kusema baada ya wachezaji 19 wa kikosi cha kwanza cha Sporting Cp kusimamishwa kuitumikia timu hiyo baada ya kujaribu kumpinga raisi wa timu hiyo.

Chanzo cha sakata hili ni Athletico Madrid, baada ya Athletico Madrid kuwafunga Sporting Cp mabao 2 kwa 0 hali ambayo iliamsha hadira kwa raisi wa Sporting Bruno de Carvalho na kuamua kuwashambulia wachezaji wake.

Kupitia mtandao wa FaceBook raisi huyo alioneshwa kukerwa kwa kile alichosema kutojituma kwa wachezaji wake na kusema hawajitolei kwa ajili ya timu na ndio maana wanafungwa kirahisi.



Raisi huyo amesema kwamba aina ya timu anayotaka kuwa nayo ni timu ambayo wako 11 uwanjani lakini wawe wanacheza kama wako 22 hali ambayo wachezaji wa Sporting CP hawaioneshi na hawakabi wala kufunga.

Baada ya ujumbe huo wachezaji 18 wa Sporting Cp waliamua kuutuma mitandaoni na kuonesha kutoridhishwa na kile alichofanya raisi wao na hapo ndipo raisi aliamua kuonesha nguvu yake ya uongozi.

Wachezaji 19 ikiwemo nyota Rui Patricio, William Carvalho, Fabio Coentrao, Bruno Fernandes, Gelson Martins, Bryan Ruiz, Sebastian Coates walisimamishwa, na kupitia tena ukurasa wa facebook raisi huyo amesema hatua zaidi zitakuchukuliwa.

JERRY TEGETE ATOA NENO KUHUSU MAJIMAJI KUSHUKA DARAJA

$
0
0



Ongeza kichwa

anaamini wataendelea kupigana na ikiwezekana kuikoa timu hiyo.
Katika mchezo uliopita, Majimaji ilifungwa mabao 3-2, wikiendi iliyopita jana, ilipokutana na Mwadui FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo ibaki mkiani ikibaki na pointi 16 baada ya kucheza mechi 23.
“Kwa kweli anko hali ni mbaya lakini bado hatujakata tamaa, tutaendelea kupigana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha tunainusuru timu isishuke,” alisema straika huyo wa zamani wa Yanga ambaye ni mwenyeji wa Mwanza.
by richard@spoti.co.tz

TAZAMA BAADHI YA RECORD KUBWA KWENYE MPIRA WA MIGUU DUNIANI.

$
0
0
Tumekuletea baadhi ya record kubwa kuwahi kutokea katika mchezo wa soka ulimwenguni kote tazama video hapa chini.

Okwiiiiii aizamisha Mtibwa

$
0
0

Morogoro. Mshambuliaji Emmanuel Okwi amefunga bao lake 17 msimu huu akiiongoza Simba kuichapa Mtibwa Sugar 1-0 katika mchezo Ligi Kuu uliomalizika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Ushindi huo unaifanya Simba kuongoza ligi kwa pointi 52 na kuiacha Yanga iliyokuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi sita hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Wakati Simba ikijikita kileleni naye mshambuliaji Okwi amefunga bao lake la pili nje ya Dar es Salaam msimu huu na kumfanya kufikisha mabao 17 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kunyakuwa tuzo ya mfungaji bora msimu huu.
Okwi alifunga bao lake katika dakika 23, akiunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na John Bocco aliyepokea krosi ya Kichuya na kutegeneza nafasi hiyo iliyomkuta Mganda huyo aliyeumbukiza mpira wavuni na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Simba waliofurika uwanjani hapo.
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na dakika ya pili, kipa wa Mtibwa, Tinoco alifanya mzaha mpira unachukuliwa na Bocco ila kabla hajafanya lolote anafanikiwa kuutoa na kuwa wa kurusha, katika tukio hilo kipa huyo aliumia na madaktari kuanza kumtiabia
Simba iliendelea kulishambulia lango la Mtibwa na dakika 4, Kapombe alipiga shuti nje ya 18, linatoka nje na dakika 12, krosi Kichuya inapanguliwa na Tinoco.
Dakika 23, krosi ya Kichuya anatua katika kichwa cha Bocco ambaye anampa pasi ya kichwa Okwi anafunga goli la kwanza kwa Simba, baada ya bao hilo Mtibwa iliamka na dakika 26, wanapata faulo inapigwa inapaa juu ya goli la Simba
Dakika ya 30, Mtibwa wanapata kona inapigwa na Kihimbwa beki wa kati Dickson anamalizia kwa kichwa inapaa juu ya goli la Simba, kasi hiyo ya mchezo inawalazimisha wachezaji wa kiungo Dilunga wa Mtibwa na Mkude wa Simba wanapewa kadi za njano baada ya kuacha mpira na kuanza kuzozana na kufanya timu hizo kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-0.
 Kipindi cha pili Simba ilirudi kwa kucheza kwa kujilinda zaidi na kuwaacha Mtibwa Sugar kutawala mchezo huo, lakini washambuliaji wake walikosa umakini katika kumalizia nafasi walizozipata.
Mtibwa iliwatoa Stamili Mbonde, Aidan, Hassan Dilunga na kuwaingiza Hussein Javu, Haruna Chanongo na Semtawa wakati Simba iliwapumzisha Mzamiru Yassin na kuingia Salum Mbonde , pia alitoka Gyan na kuingia Niyonzima
Mabadiliko hayo hayakuwa na faida kubwa kwa timu zote ziliendelea kutegeneza nafasi, lakini walishindwa kuzitumia na kufanya machezo huo kumalizika kwa Simba kushinda kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Jamhuri baada ya misimu mitatu.
PLASTA YAFUNGA NYAVU
Katika hali isiyotarajia mwamuzi Abubakar Mturo alizimika kutumia plasta kufunga nyavu za uwanjani kabla ya  kuanza kwa mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Simba.
Katika goli alilosimama kipa Aish Manula nyavu zilikuwa zimechanika na alipoona mwamuzi wa mchezo huo,   akaamua  kuzifunga ili kuepusha kusitokee hitalafu  katika mchezo huo unaoonekana kuwa mgumu,  Simba ikiwa inasaka  kuendelea kukaa kileleni.
Zoezi la kufunga nyavu hizo likiendelea kipa wa Simba, Manula alikuwa bega kwa bega kuhakikisha anakula salama  katika lango lake.
Msimamo Ligi Kuu  Bara 2017/2018
                          P W     D       L        F       A       PTS
1. Simba        22         15     7       0       52     11     52
2. Yanga         21        13     7       1       38     11     46
3. Azam         23         12     9       2       24     10     45
4. Prisons       23        9       10     4       22     15     37
5. Singida     23          9       9       5       21     21     36
6.Mtibwa     22          7       9       6       18     16     30
7. Lipuli         23         6       10     7       16     17     28
8.Mbeya       23         5       11     7       20     25     26
9. Ruvu           23        6       8       9       20     29     26
10. Stand        23       6       7       10     15     26     25
11.Mwadui    23       4       11     8       24     30     23
12.Ndanda    23        4       11     8       16     22     23
13.Kagera      23        4       10     9       14     23     23
14.Mbao        23       4       8       11     19     30     20
15.Njombe     23       3       9       11     13     31     18
16.Majimaji    23      2       10     11     18     32     16

Chanzo: Mwanaspoti
Viewing all 699 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>