Quantcast
Channel: SPOTI Starehe™
Viewing all 699 articles
Browse latest View live

Yanga wapewa mbinu hii kuimaliza Welayta Dicha ya Ethiopia

$
0
0
Kocha mkuu wa klabu ya Zimamoto ya Zanzibar ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi wa chama cha soka Zanzibar (ZFA) adbulan Msoma ametoa ushauri wa bure kwa Yanga kuhusu  wapinzani wao Wolaitta Dicha kabla ya mechi yao ya kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika.
Msoma anaifahamu Wolaitta Dicha baada ya kucheza na timu yake msimu huu lakini Zimamoto iliondoshwa kwenye mashindano baada ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Zanzibar kabla ya kufunga 1-0 kwenye mechi ya marudiano huko Ethiopia.
“Wolaitta Dicha kwa uzoefu wangu wa kufundisha timu zilizocheza mashindano ya Afrika, ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo lakini maajabu ni kuona imefika hadi hatua hii.”
“Ni timu ambayo inategemea wachezaji wawili (nahodha wao ana rasta na kiungo mmoja anatumia mguu wa kushoto anavaa jezi namba 17) hao wanaweza kuwa tishio kwa timu yoyote.”
“Wachezaji wengine ni wa kawaida kabisa tena dhaifu kabisa, walinzi si wazuri kwa vichwa hawaangalii watu wanaangalia mpira ni suala la kufunga magoli tu, mie nimekosa magoli manne hapa Unguja na kule kwao nimegongesha mwamba mara mbili kwa sababu si wachezaji wanaojua kikamilifu wanachofanya uwanjani.”
“Ni wazuri kwa pasi fupifupi kwenye eneo la kiungo kwa hiyo kama mnafata mpira watawapita, lakini kama timu inawashambulia wanakuwa hawana la kufanya. Halafu ni timu dhaifu pembeni kwa hiyo nafasi ya timu kama Yanga naiona ni kubwa ikiwa watatumia mapungufu hayo.”
“Kiufundi waende mapema kwa sababu Ethiopia ipo juu na wale hawapo Addis Ababa wapo Awasa, wakifika Addis Ababa labda watalala siku moja halafu watasafiri kwa ndege kwa muda wa nusu saa wanafika kwenye huo mji wao.”
“Uwanja sio mzuri (pitch) kwa hiyo waende mapema kama siku nne au tatu wapate uzoefu wa hali ya hewa.”
Source: Shaffih Dauda
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Huyo kamusoko anataka mashabiki tuu

$
0
0
Kiungo wa Yanga thabani kamusoko anataka nguvu ya mashabiki wa timu yao siku ya Jumamosi wakati Yanga itakapokuwa inacheza nyumbani dhidi ya Wolaitta Dicha mchezo wa mtoano kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.
Kamusoko amesema kipindi hiki ambacho timu ipo kwenye wakati mgumu wachezaji wanahitaji zaidi sapoti ya mashabiki kuliko kitu kingine.
“Timu inapokuwa haifanyi viruri ndiyo inahitaji sapoti kubwa ya mashabiki kwa hiyo nawaomba mashabiki waje kwa wingi kuisapoti timu yao kwa sababu bila wao inakuwa ngumu kwa wachezaji. Kwa sasa timu ipo katika kipindi kigumu na ndiyo hali ya mpira, timu haiwezi ikawa inashinda kila siku”-Thabani Kamusoko amezungumza na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’ mjini Morogoro.
Mchezaji huyo raia wa Zimbabwe amesema mchezo wa jumamosi utakuwa mgumu hivyo wanahitaji kuwaheshimu wapinzani wao kwa hatua waliyofika.
Mashindano ya Caf magumu kwa sababu ukiona timu imefika hatua ambayo ikicheza mechi mbili ikishinda inaweza kuingia hatua ya makundi sio ya kuichukulia poa, Caf ni mashindano makubwa sana. Sisi tumejiandaa vizuri, tunajua timu tunayokutana nayo iko vipi tumefanya mazoezi kwa ajili ya mechi ya Jumamosi ili tuingie tena hatua ya makundi.
Amesema pia kwa sasa anapambana kuhakikisha anarejea kwenye kiwango chake baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.
“Majeraha sio mazuri, ukikaa muda mrefu bila kucheza mpira huwezi kurudi mara moja kwa hiyo unarudi taratibu hadi ifike kipindi wewe mwenyewe unaona umekaa sawa. Nimerejea lakini najitahidi nirudi kwenye kiwango changu naamini taratibu nitakuwa poa.”
Source: Shaffih Dauda
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Yanga kuwasili Dar leo na dozi ya Waethiopia

$
0
0

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuwasili jijini Dar es Salaam leo tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC kutoka Ethiopia.

Yanga iliweka kambi mjini Morogoro kufanya maandalizi ya kuwawinda Waethiopia hao ambao tayari wameshawasili nchini tangu Jumanne ya wiki hii.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza utafanyika katika Uwanja wa Taifa kesho Jumamosi kuanzia saa 10 kamili jioni.

Taarifa zilizotoka CAF zimeeleza kuwa Yanga itawakosa wachezaji Papy Kambamba, Kelvin Yondan, Said Makapu na Obrey Chirwa ambao wana kadi mbili za njano kwa kila mmoja.

Tayari uongozi huo umesema utafanya mawasiliano na CAF kupitia TFF ambapo umeeleza kwa rekodi zao unaonesha Yondani hakuwa na kadi mbili, bali alipata moja pekee

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

PANCHA: Ngoma aumia tena mazoezini jioni

$
0
0
Mshambuliji wa timu ya Yanga, Donald Ngoma ameumia tena mazoezini na hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza kesho na Wolaita Dicha katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika.

Ngoma alisafiri na wachezaji wenzake kuelekea mkoani Singida katika mchezo wa robo fainali ya kombe la FA waliotolewa na Singida United, Aprili mosi baada ya kupona majeraha yake.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa amesema wamemuengua Ngoma katika mchezo huo kutokana na kupata tena maumivu hivyo wachezaji wengine wataziba nafasi yake.

"Ngoma ameumia tena na hatokuwa sehemu ya mchezo wa kesho mpaka atakapokuwa fiti kabisa," alisema Nsajigwa.

Ngoma amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na maumivu ya goti ambapo alicheza mechi chache za mzunguko wa kwanza wa ligi wakati wa pili hajagusa hata moja.

Mbali na Ngoma wachezaji wengine wakatakao kosa mchezo huo ni pamoja na Amiss Tambwe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu, Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Said Makapu na Obrey Chirwa ambao wanatumikia adhabu ya kadi.

Source:Yanga SC
Na: Agape Patrick
Email:agape@spoti.co.tz

Habari kubwa za Magazeti ya TZ leo Jumamosi April 7, 2018 Udaku, Michezo na Hardnews

$
0
0
 Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania Jumamosi April 7, 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa


















Harmonize Afungukia Kuvunjika Kwa Mahusiano Ya Zari na Diamond

$
0
0

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize kwa mara ya kwanza amefungukia suala la kuvunjika kwa Mahusiano ya Zari na Diamond Platnumz.

Miezi miwili iliyopita siku ya wapendanao Zari alitumia ukursa wake wa Instagram kumwaga aliyekuwa mpenzi wake Diamond baada ya kuzidisha michepuko ingawa suala hilo lilitokea muda mrefu uliopita lakini mpaka leo linatrend.

Harmonize mbali ya kuwa msanii wa Diamond lakini pia ni mtu wa karibu ambaye pia alikuwa na ukaribu na Zari kwaiyo alipoulizwa anachukuliaje wawili hao kuachana alisema anaheshimu maamuzi ya Zari.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Funiko Base ya Radio Five, Harmonize amefunguka na kusema kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa sababu ana maamuzi yake binafsi.

"Mimi naheshimu sana maamuzi ya mtu siwezi kuongea kama ni vibaya au ni vizuri Kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu Mahusiano Yake ndio sina”.

Lakini pia Harmonize alisisitiza kuwa hawezi kumuongelea sana Zari na kuorodhesha mambo ambayo alimsaidia kwani unaweza ukaonekana mnafki. 
Chanzo: Udakuspecially

Nisingekua hapa bila ya Kanumba- Rose Ndauka

$
0
0

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Rose Ndauka amefunguka na kudai bila ya mafundisho na ushauri aliyopewa hapo awali na marehemu Steven Kanumba, muda huu watanzania na watu wengine wasingeweza kumtambua kama mmoja wa wasanii wazuri.
Ndauka ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo na kusema Tanzania na dunia kiujumla itaendelea kumkumbuka marehemu Kanumba kutokana na ubora na uzuri wa kazi zake alizokuwa akifanya.
"Ushauri wako bado naufatisha. Waswahili husema rafiki wa kweli sio yule atakae kupa samaki ukiwa na njaa bali ni yule atakae kufundisha kuvua samaki ili kesho uweze kukidhi mahitaji yako hata ukiwa mwenyewe pia uweze kuambukiza ujuzi huo wengine. Ulinifunza vyema, nisingekua hapa umekua sababu kubwa ya hapa nilipo. Tutakukumbuka Daima na milele... 'Rest In Peace Teacher", amesema Ndauka.
Rose Ndauka ametoa hisia zake hizo kwa jamii ikiwa leo siku ya kumbukumbu ya kifo cha marehemu Steven Kanumba. Aliyekuwa nguli wa bongo 'movies' ndani na nchi na nje ya mipaka ya Tanzania.
Chanzo: EATV

Kisa Simba Chirwa arejea kwao Zambia

$
0
0
Jumatano wiki hii straika wa Yanga, Obrey Chirwa alienda kwao Zambia kutokana na matatizo ya kifamilia, sasa uongozi wa klabu hiyo umesema mchezaji huyo anarudi muda wowote kuanzia sasa kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.

Chirwa hatacheza mechi ya leo ya Yanga dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwani ana kadi mbili za njano, hivyo kwa mujibu wa kanuni hatocheza.

Chirwa alipata kadi hizo katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers ya Boswana.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa, Chirwa atarejea baada ya wiki moja ili kuwahi maandalizi ya mechi dhidi ya Simba itakayochezwa Aprili 29, mwaka huu.

“Chirwa aliondoka kwa ruhusa ya wiki moja kwenda nyumbani kwao kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia, hatutarajii akae sana huko kwa kuwa anatakiwa awahi kurudi kwa ajili ya maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Simba,” alisema Ten. 

Chirwa ana mabao 12 kwenye Ligi Kuu Bara, na amekuwa msaada mkubwa kwa Yanga kutokana na uhodari wake wa kuzifumania nyavu.

CHANZO: CHAMPION
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Kumbe nsajigwa alimfuata chirwa jukwaani

$
0
0
Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, leo alilazimika kukaa jukwaani kukitazama kikosi cha Yanga kikipambana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha FC.
Nsajigwa hakuwa na namna ya kukaa kwenye benchi la ufundi kutokana na kutumikia adhabu ya kadi ambayo alipewa wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers FC huko Botswana.
Kocha huyo aliungana na wachezaji wake ambao wana adhabu ya kadi mbili za njano, Papy Kabamba, Obrey Chirwa aliyerejea leo kutoka Zambia, Kelvin Yondani pamoja na Said Makapu.
Kukaa jukwaani kwa Sanjigwa pamoja na wachezaji waliokuwa wana kadi mbili za njano, kumeipusha Yanga kupatwa na msala mwingine wa adhabu, ambapo sasa watakuwa huru kutumika kwenye michezo ijayo.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Habari kubwa za Magazeti ya TZ leo Jumapili April 8, 2018 Udaku, Michezo na Hardnews

$
0
0
 Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania Jumapili  April 8, 2018kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.














Mechi ambayo Juma Abdul hatoisahau na alichosema kabla ya mechi ya leo

$
0
0

Juma Abdul ni miongoni mwa walinzi wa pembeni wa kutumainiwa kwenye kikosi cha Yanga, ni mchezaji mwenye uzoefu ambaye ameshacheza mechi nyingi kubwa za kitaifa na kimataifa akiwa na klabu yake au timu ya taifa.
Juma ameweka wazi mechi ambayo hatoisahau katika historia yake ya kucheza soka licha ya
kukumbana na mechi nyingi lakini kuna mechi ambayo inabaki katika kumbukumbu zake.
“Nimecheza mechi nyingi na zote zilikuwa ngumu, lakini mechi siwezi kuisahau ilikuwa dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola tukafanikiwa kupita kwenda hatua ya makundi kwa sababu ilikuwa na mshikemshike kama vita. Ilikuwa imeandaliwa vizuri sana polisi, mashabiki, TFF wote walikuwa kitu kimoja.”
Kesho Jumamosi Yanga itaiwakilisha Tanzania kwenye mechi ya kimataifa katika kombe la shirikisho Afrika itakapokuwa ikicheza dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwenye uwanja wa taifa.
Juma Abdul amezungumzia pia mchezo huo pamoja na umuhimu wa mashabiki kuishangilia timu yao inapocheza katika uwanja wa nyumbani.
“Kambi yetu inaendelea vizuri namshukuru Mungu wachezaji wote wanaendelea vizuri baadhi ya wachezaji wenye kadi wamesharuhusiwa wako nyumbani lakini naamini kwa kuongezeka wachezaji wengine ambao walikuwa na majeraha nina hakika tutafanya vizuri katika mchezo Jumamosi.”
“Mechi kubwa kama hizi ni vizuri kuanzia ugenini kwa sababu ukianzia ugenini unaweza kumsoma mpinzani ili ukirudi kwenye uwanja wa nyumbani umalize mechi. Kikubwa ninachoomba kutoka Yanga (wachezaji, benchi la ufundi, uongozi na mashabiki) mechi hii tuifanye kama fainali tupambane hapa nyumbani ili tupate ushindi mzuri.”
“Mashabiki wetu wa Yanga tunawaomba wajitokeze kwa wingi kwenye mechi kwa sababu kuja kwao kwa wingi uwanjani ndio kunaweza kutupa morali sisi wachezaji kwamba watu wole waliopo uwanjani wanataka kitu kutoka kwetu sisi wachezaji tuliopo ndani ya uwanja na kutatufanya tupigane kufa na kupona kutafuta ushindi.”

Source: Shaffih Dauda
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Yanga yawatafuna wa Ethiopia 2:0 Chirwa akiwa jukwaani

$
0
0


Kikosi cha Yanga kimeanza vema hatua ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolaitta Dicha SC kutoka Ethiopia.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ulianza kutikiswa nyavu zake kupitia Raphael Daudi, mapeka kwenye dakika ya 1.

Bao hilo moja lilidumu mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika ambapo Yanga walikuwa wanaongoza.

Baada ya kipindi cha pili kuanza, Emmanuel Martin aliipatia tena Yanga bao la pili kwa njia ya kichwa na kudumu kwa dakika zote zilzokuwa zimesalia.

Mpaka Mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho, Yanga 2-0 Wolaitta Dicha SC.

Mchezo wa marudiano utafanyika huko Ethiopia wiki moja baadaye.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Sababu iliyomfanya Kamusoko ajifunze kiswahili

$
0
0
Jambo ambalo hutakiwi kufanya ni ‘kumteta’ Thabani Kamusoko kwa lugha ya Kiswahili ukiamini ni raia wa kigeni na hatoelewa unachozungumza, utakuwa umefeli jamaa ni anatwanga kiswahili hadi cha mtaani.
Kiungo huyo wa Yanga toka Zimbabwe anapozungumza Kiswahili huwezi kujua kama si raia wa

Kamusoko yupo vizuri kwa Kiswahili asikwambie mtu.
Wakati anafanya mahojiano na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’ mjini Morogoro ambako Yanga iliweka kambi kujiandaa na mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Wolaitta Dicha, alisema hakuna mwalimu aliyekuwa akimfundisha bali aliamua tu mwenyewe kujifunza Kiswahili.
Katika mazungumzo hayo, Kamusoko akafunguka sababu kubwa iliyomfanyabaamue kujifunza Kiswahili, kumbe ni ishu ya kumrahisishia mawasiliano awapo kazini akisukuma gozi.
“Mpira unahitaji mawasiliano kwa kiasi kikubwa, pia unahitaji kuzungumza lugha moja kwa hiyo niliamua kujifunza Kiswahili ili tuelewane vizuri”-Thabani Scara Kamusoko kiungo Yanga SC.
Hivi karibuni Method Mwanjale ni mchezaji mwingine ambaye anatoka Zimbabwe aliyekuwa anazungumza Kiswahili kwa ufasaha ukiachana na akina Niyonzima, Tambwe, Mavugo ambao nchi zao zinazungumza pia Kiswahili.

Source: Shaffih Dauda
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.cotz

Onesha ujuzi wako: Bao la CR7 dhidi ya Juventus linaitwaje kitaalamu?

$
0
0

Bao la mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, lililowafurahisha hata mashabiki wa Juventus, licha ya ukweli kwamba kufungwa kunauma lakini mashabiki hao wa Juventus walisimama na kumpigia makofi CR7 kwa goli hilo maridhawa.

Buffon ampongeza Ronaldo kwa kumfunga goli matata!

Na hata goli kipa wa Juventus mkongwe Buffon mwishoni mwa mchezo alimpa Ronaldo mkono wa kumkubali katika mechi hiyo ya  Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. swali ni hivi bao hilo lilikuwa bao la aina gani? yaani linaitwaje kitaalamu.

Na: sabby@spoti.co.tz

Chelsea yashindwa kutoa zawadi ya pasaka kwa mashabiki wake

$
0
0





Mabingwa wa epl msimu 2017/2018  chelsea fc wameendelea kukumbwa na vipigo mfululizo baada ya kukubali kipigo cha magori 3 kwa moja kutoka  kwa Tottenham Hotspur .mabingwa haw wamekua katika msimu mbaya baada ya kushuhudiwa wakipoteza mechi muhimu na kupunguza matumaini ya kumaliza katika nafasi nne za juu na kushiriki ligi ya mabingwa ulaya

TCRA Yatoa Hukumu kwa Times Fm Kisa Diamond. Clouds Nayo Yapewa Onyo Kali

$
0
0

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),imetoa hukumu kwa vituo viwili vya radio vya Times FM na Clouds FM kwa makosa ya ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam imesema kuwa Radio ya Times FM walitangaza mahojiano na mwanamziki Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinum.

Imeelezwa kwenye mahojiano hayo mwanamuziki huyo alitamka maneno yasiyofaa kimaudhui akimshambulia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza.
"Times FM wamepewa onyo na kutakiwa kumuomba radhi Naibu Waziri Shonza na jamii kwa ukiukwaji huo wa maadili ya utangazaji,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Kuhusu Radio ya Clouds FM ni kwamba imepewa onyo kwa kutozingatia mizania ya utoaji wa habari uliohusu pande mbili ya mwanamuziki Ibrahim Musa a.k.a Roma mkatoliki na Naibu Waziri Shonza.
Chanzo: Udaku Special 

Simba ‘ikikaza’ kidogo tu safi!

$
0
0

KIRAKA wa Simba, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wachache waliokuwepo wakati Wekundu hao wakitamba kimataifa kabla ya kupotea na kubatizwa jina la ‘Wamatopeni’.
Sasa jamaa ameapa kuwa, kwa uzoefu alionao kama wachezaji wote watakaza kidogo tu basi ubingwa msimu huu unatua Msimbazi.
Pia, amesema kwa hali ilivyo kwa sasa hawataki kupoteza mchezo na kwamba, kila mechi kwao ni fainali.
Kapombe, ambaye aliichezea Simba 2011 hadi 2013 kabla ya kutimkia Ufaransa na baadaye kurudi wakati Simba ikipoteza mwelekezo na kushindwa kubeba mataji.
Sasa Kapombe amekiangalia kikosi chao na kusema, kuna wachezaji wengi mahiri na wenye uwezo mkubwa kuhimili ushindani hivyo wana uhakika wa kubeba taji.
“Nina uzoefu wa kutosha najua nyakati pia, kwa timu ambayo tuko nayo tuna kila sababu ya kuwa mabingwa. Kuna wachezaji wenye uzoefu wa kutisha kila mmoja akiwa amecheza si chini ya misimu minne na morali ipo juu akitamani ufalme huo,” alisema Kapombe ambaye alirudi nchini mwaka 2014 akajiunga na Azam na 2017 akarudi tena Simba anayoichezea sasa.
“Ligi ni ngumu lakini unaona Simba inapambana kusaka ubingwa na jambo la muhimu ni kutodharau mechi zote kuanzia sasa hadi tunamaliza ligi,” alisema.
Simba ndiyo vinara wakiongoza na pointi 49 kisha Yanga yenye pointi 46, Azam 44, Tanzania Prisons ni wa nne wana 36 sawa na za Singida United wanaoshika nafasi ya tano na majanga yako kwa timu za Majimaji, Njombe Mji na Mbao FC ambao wanapishana kwenye nafasi za mkiani.
Simba imebakiza michezo na Mtibwa kesho Jumatatu, Yanga, Singida United, Mbeya City, Tanzania Prisons, Ndanda, Kagera Sugar, Lipuli na Majimaji.
Chanzo: Mwanaspoti

Huyu Wambura mbishi jamani

$
0
0

KAMA unadhani aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, amesalimu amri basi utakuwa umekosea sana aisee. Unaambiwa hivi, Wambura ambaye rufani yake kupinga kufungiwa kujihusisha na soka maisha, imetupiliwa mbali na Kamati ya Rufani na Maadili ya TFF, ameapa kuendelea kupambana na kusisitiza kuwa hajakubali.
Jana, Wambura amezungumzia uamuzi wa Kamati ya Wakili Ebenezer Mshana, akisema ulikuwa ni mkakati wa kubariki mtu kuchafuliwa na kusema kamwe hatakubali na anajipanga upya kwa mapambano.
Kauli hiyo ya Wambura inakuja ikiwa ni siku moja tangu Wakili Mshana kutangaza uamuzi wa kamati yake kubariki hukumu ya Wambura kufungiwa maisha iliyotolewa awali na Kamati ya Maadili.
Akitumia dakika 42 kufafanua mambo mbalimbali kuhusiana na uamuzi wa Kamati ya Wakili Mshana, Wambura alisema bado hajapatiwa haki yake ya msingi ya kusikilizwa.
Mdau huyo wa soka, ambaye ana sifa ya kupambana linapokuja suala la kudai haki yake, alisema anasubiri nakala ya hukumu hiyo na baada ya hapo ataketi na timu ya wanasheria wake kuangalia ni mlango sahihi wa kuutumia ili kupata haki yake.
Aliwataka Watanzania na wapenda soka kutulia na kamwe wasiwe na shaka kwa kuwa, anafahamu njia sahihi za kupata haki yake. Pia, amesema kilichofanywa na kamati hizo mbili za TFF ni kutokana na mapambano yake na atatumia shauri hilo kubadili zaidi kanuni za soka la Tanzania ili kila mdau apate haki. “Mpaka sasa haki tunayoipigania hatujaipata kwani, tunataka kupatiwa nafasi ya kusikilizwa na bado tunaona hatujasikilizwa, wanasema wana ushahidi kwanini hawataki tuweke mambo hadharani?,” alihoji Wambura.
“Tuliomba hii kesi isikilizwe kama mahakama ya wazi (open court) hawataki, lakini hukumu yao jana (juzi) wameitoa ikiwa mubashara, tunachotaka Watanzania waone kila kitu ili wawe mashuhuda na kinachoendelea ndani ya TFF,” alisema na kuongeza:
“Wanataka mtu aonekane mwizi, fisadi na wanadai nina kesi ya Simba pale Kisutu wakati ilishafutwa zamani, hilo limetoka wapi. Wamejifungia wenyewe na kutoa uamuzi wa upande mmoja, haiwezekani tutaendelea kutafuta haki yetu mbele. Haya ni mambo ya kimkakati tu.” Awali, Mwanasheria anayemtetea Wambura, Emmanuel Muga alisema ameshangazwa na hatua za kudanganya umma iliyofanywa na kamati hiyo akisema, wamezungumza mambo ya uongo dhidi yake. “Wameamua kwa makusudi kudanganya umma, akisema eti nilimuombea mteja wangu apunguziwe kifungo kitu hicho nawezaje kukifanya kama wakili? “Kuna mambo mengi yamefanyika ambayo kwetu ni kama ulikuwa mpango wa kupunguza haki ya upande mmoja, angalieni walivyobadilisha wajumbe wa kamati siku chache kabla ya kusikilizwa kwa kesi hii, hii kamati haitakiwi kubadilishwa kama walivyofanya,” alisema.
Chanzo: Mwanaspoti

Ronaldo afananishwa na mvinyo

$
0
0
Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri amemfananisha Cristiano Ronaldo na kinywaji cha mvinyo akisema kuwa kadiri umri unavyokwenda ndio anazidi kuwa mkali zaidi. Allegri alimkubali Ronaldo baada ya kuiongoza Real Madrid kuirarua Juventus 3-0 mbele ya mashabiki wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wiki iliyopita.
“Unajua Ronaldo yaani ni sawa na mvinyo kadiri muda unavyokwenda ndio anazidi kuwa bora,” alisema Allegri baada ya mchezo huo, ambao Ronaldo aliacha mashabiki wa soka mdomo wazi baada ya kufunga bao maridadi la ‘tik tak’. Allegri alisema kuwa Ronaldo amekuwa straika bora wa dunia kwa miaka miwili sasa.
 Alisema kuwa pamoja na fowadi huyo kuwa na umri wa miaka 33 lakini bado ana kiwango cha kutisha. Nyota ya Ronaldo bado ipo juu Real Madrid wakati wenzake waliounda kombinesheni ya BBC yaani Gareth Bale na Karim Benzema wakiwa wamechuja siku za karibuni. 
Katika miaka ya nyuma, Ronaldo alikuwa anasifika kwa mbio na chenga lakini kutokana na umri kumtupa mkono siku hizi anahakikisha anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kila mara.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Kichuya apewa jukumu hili zito

$
0
0

Baada ya kufanikiwa kuivuruga Singida United juzi, Mtibwa Sugar wamesisitiza kwamba hizo ni salamu tosha kwa Simba na kuwataka wajiandae kisaikolojia. 

Lakini kocha kijana wa Simba anayekubalika zaidi na mashabiki, Masoud Djuma amewaambia kwamba majibu yatapatikana uwanjani huku wakimpa majukumu Shiza Kichuya.

Mtibwa yenye pointi 30, inawakaribisha Simba kesho Jumatatu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ikiwa imeshinda michezo yake miwili mfululizo ule wa FA dhidi ya Azam FC na wa ligi baina ya Singida United timu ambazo zote zinaongozwa na makocha wa kigeni huku wao wakiongozwa na mzawa Zuber Katwila.

Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru anasema; “Kwa sasa Mtibwa ipo vizuri ndiyo maana hata Simba hawana raha sababu wameingia na hofu kutokana na kasi yetu ambayo tumeonyesha kwenye michezo miwili ambayo
imepita hivyo hawalali huko wanawaza waje na mbinu gani.”


“Sababu tumeweza kuzifunga timu mbili na zote mabenchi yao ya ufundi yapo na makocha wageni na wachezaji wa kigeni na tunaenda kukutana na Simba nao wakiwa hivyo hivyo. Hatuna kisingizio, tutawapiga.”

Beki wa kati wa Mtibwa, Cassian Ponela ameeleza kuwa; “Sisi kwa upande wetu kama mabeki, tumeshapeana majukumu ya kuhakikisha hao washambuliaji wao tunawazuia ili tufikie malengo.


” Kichuya apewa majukumu Straika mwenye mizuka ndani ya Simba, Shiza Kichuya amekabidhiwa majukumu mazito na kocha mkuu wa timu hiyo, Mfaransa, Pierre Lechantre kuhakikisha anaimaliza Mtibwa.

Lechantre ambaye CV yake ni kubwa kuliko makocha wote nchini, anaamini katika mechi ya kesho washambuliaji wake John Bocco pamoja na Emmanuel Okwi, watawekewa ulinzi mkali hivyo ni jukumu la wachezaji wake wengine akiwemo, Kichuya kuhakikisha wanafanya mambo.

“Mtibwa Sugar watakuja uwanjani kwa lengo la kuhakikisha Okwi na Bocco hawapati nafasi ya kucheza kabisa lakini wapo wengine kama vile Kichuya nimewapa majukumu ya kufanya pindi hali hiyo itakapojitokeza ili tuweze kupata ushindi,” alisema Lechantre.

CHANZO: SPOTI XTRA
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
Viewing all 699 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>