Quantcast
Channel: SPOTI Starehe™
Viewing all articles
Browse latest Browse all 699

DALALI: Ubingwa simba ni uhakika 100%

$
0
0




































Na George Mganga
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, anaimani timu yake itatwaa ubingwa wa ligi msimu huu baada ya kuukosa kwa muda wa takribani miaka mitano.
Dalali ambaye aliwahi kufanya vizuri wakati akiwa Mwenyekiti wa Simba, amesema kikosi walichonacho hivi sasa kina morali ya juu na si kama kama kadhaa nyuma.
"Simba hii iko vizuri, hauwezi ukailinganisha na timu zingine katika ligi, uwezekano wa kubeba kombe upo kwa asilimia 100" alisema Dalali wakati akizungumza na kipindi cha Michezo, kupitia Radio One jana.
Aidha Dalali ametamba kwa kusema Simba ni lazima ishinde mchezo wa Jumanne dhidi ya Njombe Mji ili kuendelea kujitengenezea mazingira ya kuwa kileleni. Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Dalali ameeleza mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuwa na uhitaji wa alama tatu, hivyo watambana ili kupata matokeo.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

Viewing all articles
Browse latest Browse all 699

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>