Ombi la nchi ya Morocco kuwa taifa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia 2026 imechukua hatua mpya baada ya shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kutuma wawakilishi wake nchini Morocco.
Wawakilishi hao wa FIFA wamewasili nchini Morocco hapo jana Jumatatu kwa ajili ya kukagua baadhi ya mambo ili kuipa nafasi Morocco kweza kuanza kuandaa michuano hiyo mikubwa zaidi ulimwenguni.
Morocco ndio taifa pekee kutoka barani Africa ambalo limetuma ombi la kuandaa michuano hiyo lakini watakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa mataifa mengine kama Mexico, Canada na Marekani ambao nao wanaitaka.
Hii itakuwa mara ya tano kwa Morocco kuomba kuandaa michuano hii kwani 1994 walishuhudi ikienda kwa Marekani, wakajaribu tena 1998 ikaenda kwa Ufaransa na wakajaribu tena 2010 na likaenda kupigwa South Africa.
Timu ya watu 5 kutoka FIFA iliyoko Morocco itafanya kazi yake kuanzia leo tarehe 17 hadi tarehe 19 na baada ya hapo watarudisha taarifa FIFA na kisha kusubiri maamuzi ya FIFA yatakayotolewa June 13 mjini Moscow.
Chanzo: Shaffih Dauda