Ama kila jambo lina nyakati zake, kila jambo lina majira yake! Alitukana, aliwachamba wanawake wenzie waliowahi kumvulia nguo mzazi mwenzie, a.k.a Simba, - The boy from Tandale, nadhani alipata jeuri hiyo ya kuwasema vibaya wanawake wenzie kwasababu kamzalia watoto wawili! Huyu si mwingine bali ni Zari, a.k.a The Boss lady .
Wanaume ni viumbe vya ajabu sana! Ama tuseme Diamond ni kiumbe wa ajabu sana! pamoja na kumpatia watoto wawili lakini ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua wapendanao na wazazi hao wakaachana! Leo Diamond tayari anaonekana anayafurahia maisha yake bila mzazi mwenzie huyo.
Uchungu anaoupata Zari hauwezi kupimika! maana inatia hasira kuachana na mpenzi wako na kuendelea kumuona akifurahia maisha!
sabby@spoti.co.tz