Habari za udaku mitaani zinasema yule mtangazi anaejiamini kuwa ni mzuri kuliko na mwenye shape nzuri kuliko watangazaji wote Africa mashariki na kati Diva "loveness" ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha mahaba (Ala za nafsi) Clouds Fm ametundikwa mimba na mtangazaji mwenzie Michael Lukindo a.k.a "informer" hizi ni tetesi, na sie waswahili huwa tunasema: lisemwalo lipo kama halipo linakuja, lakini kwa hili msemo huo unafaa ubadilike na iwe: Lisemwalo hakika lipo! Ujauzito ni kama pembe la ng'ombe, halifichiki! Muda utaongea.
Inasemekana kijana informer alitumia ule mwanya wa Diva kubwagwa hadharani na kugeuka kama mfariji wake na mwisho wa siku wakaangukia kwenye mapenzi huku wakifanya kazi ktuo kimoja...Ama kwa hakika "Penye uzia penyeza Rupia" waswahili walinena.
Baada ya muda Diva alimwambia informer kuwa nina mimba na ndugu Michael alipokea habari hiyo kwa furaha na alikuwa kwenye process za kuacha kazi na kuanza kufanya muziki kama msanii. Usichezee kuitwa baba.
Huyu 'Diva' huyu, siyo muda mrefu aliutangazia umma kwamba: eti anaetaka kumuoa lazima akalipe mahali ya thamani Tsh 500milioni! sasa nadhani shilingi yake inashuka kwa kasi sana! maana kwa kubeba kibendi inamaana huweza kushusha thamani! au wachumi mnasemaje? kajiongezea thamani au kajishushia thamani! Hongereni wazazi watarajiwa.
Na: sabby@spoti.co.tz