Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha ujumbe wa Twitter kwamba Urusi inafaa 'kujiandaa' kwa kombora litakalorushwa nchini Syria akijibu madai ya shambulio la kemikali wikendi.
Maafisa wakuu wa Urusi walitishia kujibu shambulio lolote la Marekani. Bwana Trump aliahidi kujibu vikali madai hayo ya shambulio la kemikali.
Serikali ya Bashar al-Assad ambayo hupokea usaidizi wa kijeshi kutoka Urusi imekana kuhusika na shambulio hilo la kemikali.
Katika chapisho lake la Twitter, bwana Trump alimuita rais Assad 'mnyama anayetumia gesi kuua watu'.
Siku ya Jumamosi, wanaharakati wa Syria, waokoaji na maafisa wa matibabu walisema kuwa mji huo wa Douma unaodhibitiwa na waasi katika jimbo la mashariki la Ghouta ulishambuliwa na vikosi vya serikali kwa kutumia mabomu yalio na sumu.
Shirika la matibabu linaloshirikisha mataifa ya Syria na Marekani limesema kuwa watu 500 walipatikana na dalili za kushambuliwa na kemikali. Kutokana na shambulizi hilo la kemikali Marekani na washirika wake Ufaransa na Uingereza wamekubali kufanya kazi pamoja na wanaaminika kujiandaa kutekeleza shambulio la kijeshi.
Lakini Urusi inasemaje?
Serikali ya Urusi imetaja ripoti za shambulio la kemikali kama uchokozi unaolenga kuthibitisha haki ya Ulaya kumuingilia mshirika wake, Syria.
Maafisa kadhaa wa Urusi wameonya kwamba iwapo Marekani itashambulia Syria basi Marekani ijue kwamba Urusi haitakaa kimya. Alexander Zasypkin , ambaye ni balozi wa Urusi nchini Lebanon akirejelea onyo la kiongozi wa jeshi kwamba makombora yatatunguliwa huku maeneo yanayotoka yakilengwa.
Trump, raisi ambaye ofisi yake kuu imekuwa kama imehamia katika mitandao hasa mtandao wa Twita, ameandika chapisho lake kama lilivyonukuliwa hapa chini:
Inawezekana Trump anataka kuipeleka dunia katika vita ya tatu ya Dunia? Muda utaongea!
Source:bbc
Na: Sabby@spoti.co.tz