Na George Mganga
Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Raphael Daud, jana aliweka rekodi yake katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Daud aliifungia Yanga bao la kwanza katika sekunde ya 27 tu ya mchezo, likiwa ni bao la mapema zaidi kwenye michuano hiyo msimu huu.
Bao hilo linatengeneza rekodi kwa Daudi na Yanga kwa ujumla kutoa mchezaji aliyeweza kucheka na nyavu ndani ya nusu dakika dhidi ya Wolaitta Dicha SC kutoka Ethiopia.
Yanga iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Bao jingine la Yanga lilifungwa na Mshambuliaji Emmanuel Martin kwa njia ya kichwa katika dakika ya 54 ya kipindi cha pili.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kujitengenezea mazingira mazuri ya kuingia hatua ya makundi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki moja baadaye huko Ethiopia
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz